Tuesday, February 9, 2016

EMIRATES FA CUP: LEO TENA PATASHIKA!! MARUDIANO WEST HAM vs LIVERPOOL

Baada ya kutoka Sare 0-0 hapo Januari 30 huko Anfield, Jijini Liverpool, West Ham na Liverpool sasa zitarudiana Jijini London Uwanjani Upton Park katika Mechi ya Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP.
Mshindi wa Mechi hii atasonga Raundi ya 5 na kucheza Ugenini hapo Februari 21 na Blackburn Rovers.
Mechi nyingine ya Marudiano ya Raundi ya 4 ya Kombe hili itachezwa Jumatano kati ya Peterborough na West Brom na Mshindi wake kucheza Raundi ya 5 Ugenini na Reading.


Mechi za Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP zitachezwa kuanzia Jumamosi Februari 20 na kumalizika Jumatatu Februari 22.

EMIRATES FA CUP
Ratiba
Raundi ya 4 Marudiano
Jumanne Februari 9

2245 West Ham vs Liverpool

Jumatano Februari 10
2245 Peterborough v West Brom

Raundi ya 5
Jumamosi Februari 20

1545 Arsenal v Hull
1800 Reading v West Brom au Peterborough
1800 Watford v Leeds
2015 Bournemouth v Everton

Jumapili Februari 21
1700 Blackburn v Liverpool au West Ham
1800 Tottenham v Crystal Palace
1900 Chelsea v Man City

Jumatatu Februari 22
Shrewsbury v Man United


THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016


Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016

Fainali Jumamosi 21 Mei 2016