Tuesday, February 16, 2016

EUROPA LEAGUE: ALHAMISI NI PATASHIKA, MIDTJYLLAND vs MAN UNITED, AUGSBURG vs LIVERPOOL, FIORENTINA vs TOTTENHAM SPURS!

Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI itachezwa Wiki hii kwa Mechi 16 na England ina Timu 3 ambazo ni Manchester United, Liverpool na Tottenham.
Raundi hii imejumuisha Timu 24 zilizofuzu kutoka Makundi ya Mashindano haya na Timu 8 zilizomaliza Nafasi za 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI ikiwemo Man United.
Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI itachezwa Wiki hii kwa Mechi 16 na England ina Timu 3 ambazo ni Manchester United, Liverpool na Tottenham. Timu hizi 3 za England zote zitaanza kucheza Mechi zao Ugenini hapo Alhamisi Februari 18 kwa Man United kucheza huko Denmark na FC Midtjylland, Tottenham, ambao walishiriki Mashindano haya kutoka hatua ya Makundi, wamepangiwa Klabu ya Serie A Fiorentina wakati Liverpool, ambao pia walikuwemo Makundi ya EUROPA LIGI, watacheza na Klabu ya Germany Augsburg.
Valencia ya Spain, ambayo ipo chini ya Mchezaji wa zamani wa Man United Gary Neville, watacheza na Rapid Vienna ya Austria wakati mtanange mkali wa Raundi hii ni ule wa Borussia Dortmund na FC Porto.
EUROPA LEAGUE
Raundi ya Mtoano ya Timu 32
Jumanne Februari 16

20:00 Fenerbahce v Lokomotiv Moscow

Alhamisi Februari 18

[Kuanza Saa 21:00]
Sevilla v Molde
Villarreal v Napoli
Borussia Dortmund v Porto
Anderlecht v Olympiacos
Fiorentina v Tottenham
St Etienne v Basle
Midtjylland v Manchester United
[Kuanza Saa 23:05]
Valencia v Rapid Vienna
Augsburg v Liverpool
Sparta Prague v Krasnodar
Galatasaray v Lazio
Sion v Braga
Shakhtar Donetsk v Schalke
Marseille v Athletic Bilbao
Sporting Lisbon v Bayer Leverkusen
 

Mechi za Marudiano ni Februari 25.
KALENDA
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Kwanza: 18 Februari
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Pili: 25 Februari
Raundi ya Timu 16-Droo: 26 Februari, Nyon
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi