Wednesday, February 17, 2016

EUROPA LIGI: VAN GAAL ABEBA WACHEZAJI 18 KWENDA DENMARK, WAYNE ROONEY ABAKI ENGLAND.

Louis van Gaal ametaja Wachezaji 18 watakaounda Kikosi cha Wachezaji wa Manchester United ambao Leo wanakwenda Denmark kucheza Mechi ya UEFA Europa Ligi na FC Midtjylland Alhamisi Usiku.
Kepteni Wayne Rooney hayumo kwenye Kikosi hicho pamoja na Matteo Darmian alieteguka Bega Jumamosi iliyopita walipofungwa 2-1 na Sunderland huko Stadium of Light.
Mastaa wengine ambao hawamo Kikosini ni Marouane Fellaini na Beki Chipukizi Cameron Borthwick-Jackson.

Lakini wamo Chipukizi kadhaa akiwemo Donald Love ambae Jumamosi aliingizwa kumbadili Matteo Darmian alipoumia huko Sunderland na wengine ni Will Keane, ambae ashawahi kuichezea Timu ya Kwanza pamoja na Regan Poole, Joe Riley na James Weir ambao bado wanalilia Mechi yao ya kwanza kwenye Kikosi cha Kwanza.
KIKOSI CHA MAN UNITED KILICHOENDA DENMARK:
De Gea, Romero, Love, McNair, Smalling, Blind, Poole, Riley, Carrick, Herrera, Schneiderlin, Lingard, Pereira, Weir, Mata, Memphis, Martial, Keane.
Wakitua Denmark

Michael Carrick