Saturday, February 20, 2016

FA CUP: ARSENAL 0 v 0 HULL CITY


Mabingwa Watetezi wa FA CUP Arsenal itabidi waende huko KC Stadium kurudiana na Hull City baada ya Leo kutoka Sare 0-0 Uwanjani Emirates katika Mechi ya Raundi ya 5 ya EMIRATES Fa cup.
Kila Timu ilifanyika mabadiliko makubwa katika Vikosi vyao vilivyocheza Mechi zao zilizopita kwa Arsenal kubadili Wachezaji 9 na Hull City 10 lakini Arsenal wakashindwa kuipenya ngome ya Hull huku Kipa wa Vinara hao wa Daraja la chini la Championship wakijilinda imara kwa Kipa wao, Eldin Jakupovic, kuokoa Bao kadhaa za wazi.
Katika Mechi nyingine za Raundi ya 5 ya FA CUP zilizochezwa Leo Readuing, inayocheza Championship, iliitwanga West Brom ya Ligi Kuu England Bao 3-1 baada ya kutoka nyuma kwa Bao la Dakika ya 54 la Darren Fletcher nas kubamiza 3 zao kupitia Paul McShane, Dakika ya 59, Michael Hector, 72, na Lucas Piazon, 94.
Nao Watford wameitungua Leeds United 1-0 kwa Bao la kujifunga mwenyewe Scott Wootton la Dakika ya 53.