Wednesday, February 17, 2016

FULL TIME: SPORTING GIJON 1 v 3 BARCELONA, MESSI AFUNGA BAO LA 300 NA 301 AKIFUNGA BAO MBILI LEO LA LIGA!


Wakicheza kwenye Uwanja wa Sporting Gijón El Molinón
Sporting Gijón bao lake limefungwa na Carlos Castro dakika ya  27

Barcelona bao zake zimefungwa na 
• Lionel Messi 25'
• Lionel Messi 31'
• Luis Suárez 67' 


Lionel Messi, Jana alikuwa Mtu wa kwanza katika Historia ya La Liga kufikisha Mabao 300.
Jana Barcelona waliifunga Sporting Gijon Bao 3-1 na kuongoza La Liga wakiwa Pointi 6 mbele huku Messi akipachika Bao 2.
Bao la kwanza la Messi lilimfanya afikishe Bao 300 kwenye La Liga ambako alifunga Bao lake la kwanza kabisa akiwa pia na Barcelona takriban Miaka 11 iliyopita.
Bao lake la pili kwa Barca hiyo Jana pia liliandika Historia kwani lilikuwa Bao la 10,000 katika Historia ya Klabu ya Barcelona.
Mwaka Jana Messi alimpita Telmo Zarra kwenye Ufungaji Bora katika Historia ya La Liga ambae alikuwa na Mabao 251 Rekodi ambayo ilisimama kwa Miaka 59.

Lionel Messi akipeta baada ya kufunga bao la 300 hii leo kwenye La Liga

Pongezi kwa Lionel Messi

Luis Suarez nae katupia leo

Moja kwa moja.

Luis Enrique na Meneja mwenzie wakisalimiana baada ya kukutana

Fowadi wa Brazil Neymar akipanga awatokeje

Messi akichuana na difenda  Roberto Canella leo