Saturday, February 13, 2016

FULL TIME: STAND UNITED 1 v 2 SIMBA, AMISI KIIZA AIPANDISHA SIMBA KILELENI LEO!

Amisi Kiiza alifunga bao lake la 15 msimu huu kipindi cha kwanza dhidi ya wenyeji Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage
BAO 2 za Straika kutoka Uganda, Hamisi Kiiza, Leo zimewapa ushindi wa Bao 2-1 Simba walipocheza na Stand United huko Kambarage Jijini Shinyanga na kuwapa uongozi wa Ligi Kuu Vodacom, VPL.
Simba sasa wapo kileleni wakiwa na Pointi 45 kwa Mechi 19 wakiguatiwa na Yanga wenye Pointi 43 kwa Mechi 18 na wa 3 ni Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 16.
Hadi Mapumziko, Simba walikuwa mbele 1-0 na Kipiundi cha Pili Kiiza tena kuwapa Bao la pili na mwishoni Stand United kufunga Bao lao moja.
Huko Sokine, Mbeya, Wenyeji Mbeya City waliitwanga Toto Africans Bao 5-1 kwa Bao za Rafael, Ramadhan Chombo, Boban, Bao 2 na Meshak.

Mechi inayofuata kwa Simba kwenye VPL ni Jumamosi ijayo ambapo wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza Dabi ya Kariakoo na Watani zao Yanga ambao Wikiendi hii hawana Mechi ya VPL kwa vile Leo walikuwa huko Visiwani Mauritius kucheza Mechi yao ya kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONS LIGI walipoipiga Cercle de Joachim 1-0 kwa Bao la Donald Ngoma
.