Friday, February 19, 2016

FULL TIME: UEFA EUROPA LEAGUE: FC MIDTJYLLAND 2 v 1 MANCHESTER UNITED

FC Midtjylland, Kitimu cha Denmark kilichoanzishwa Mwaka 1999 chenye Uwanja MCH Arena unaochukua Watu 11,800, Leo kimeichapa Manchester United Bao 2-1 katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya UEFA EUROPA LIGI.
Man United walitangulia kufunga lakini udhaifu wa Kiungo na Difensi yao uliruhusu FC Midtjylland kupiga Bao 2 na kuwa na nafasi kadhaa za kuongeza Bao nyingine kadhaa.
Man United, wakiwakosa Wachezaji wao kadhaa kutokana na maumivu, walipata pigo kabla Mechi hii kuanza baada ya Kipa wao David de Gea kuumia Enka wakati akipasha mwili moto na nafasi yake kuchukuliwa na Kipa wa Argentina Sergio.
Timu hizi zitaruadiana huko Old Trafford Alhamisi ijayo.