Monday, February 29, 2016

GERARD PIQUE ATOBOA YA MOYONI MWAKE! ASEMA ANA MAPENZI NA KLABU YA MAN UNITED NA HAMFUATI GUARDIOLA CITY!

Beki wa Barcelona Gerard Piqué amefuta kabisa uwezekano wa yeye kuungana na Pep Guardiola huko Manchester City mwishoni mwa Msimu huu kutokana na mapenzi yake na Klabu yake ya zamani ya Manchester United.
Mwishoni mwa Msimu huu, Guardiola atachukua wadhifa wa kuwa Meneja mpya wa Man City na kumekuwa na habari kadhaa za Mastaa kadhaa kuchukuliwa na Kocha huyo wa sasa Bayern Munich kwenda huko City mara tu akianza kazi yake mpya.
Lakini Pique yeye amejiondoa kwa wale watakaofanya hivyo kwa sababu tu ya mapenzi yake na Man United ambako alichezea kwa Miaka Minne.

Beki wa Barcelona Gerard Piqué amefuta kabisa uwezekano wa yeye kuungana na Pep Guardiola huko Manchester City mwishoni mwa Msimu huu kutokana na mapenzi yake na Klabu yake ya zamani ya Manchester United. Pique, mwenye Miaka 28, amesema: “Mapenzi yangu kwa Manchester United ni makubwa mno kwangu kusaini City licha ya kuwa Pep ni Kocha mzuri mno!”
Pique na Guardiola walikuwa pamoja huko Barcelona kabla Kocha huyo kuamua kuondoka kwa Mabingwa hao wa Spain.

Pique alianzia kucheza Timu ya Vijana ya Barca Mwaka 1997 hadi 2004 alipojiunga na Timu ya Vijana ya Man United na kuichezea hadi 2005 na kisha kupanda Kikosi cha Kwanza na kurudi tena Barcelona Mwaka 2008.