Sunday, February 28, 2016

HARMONIZE AUFUNGA MWEZI WA PILI NA BADO KAMSHIRIKISHA DIAMOND PLATNUMZ.

Dar es Salaam, Tanzania – February 29, 2016: Mwimbaji anaekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) kutoka Tanzania anayewakilisha kundi la Wasafi Classic Baby(Wcb), Harmonize ameachia wimbo wake wimbo mpya unaoitwa ‘BADO’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz.

SABABU YA KUREKODI WIMBO HUU.
Kwa singo mbili alizosikika Harmonize(Aiyola,Kidonda Changu) kwenye vyombo vya habari,jamii imekua ikimfananisha sana na Diamond kwenye uimbaji,ndipo siku moja Harmonize wakati akiimba Diamond alivutiwa na Melody ya wimbo huu na kusema hii itakua nafasi ya Watanzania kuwatofautisha kwenye uimbaji. 


KUHUSU WIMBO WA BADO.
Harmonize alikaa na Diamond akamuuliza ni msichana gani alishamuumiza kiasi kwamba hawezi kumsahau,ingawa Diamond hakumwambia ni msichana gani,lakini akamwambia hiyo ni idea(Mwanga) mzuri wa kutunga wimbo ‘mkali’ Beat ya wimbo huu imetengenezwa na Mtayarishaji(Producer) anaitwa Fraga na kabla ya kurekodi kwenye studio ya Wasafi,producer Fraga alimtumia midundo (Beat) 3 Harmonize achague,ndipo akachagua beat ya wimbo huu na kurudi Wasafi Records kwa ajili ya kurekebishwa na kuanza kurekodiwa. 


VIDEO YA WIMBO WA BADO.
Video ya wimbo huu imefanyika Afrika Kusini na Muongozaji(Director) anaitwa Nick ambaye ametengeneza video kadhaa ikiwemo Aiyola ya Harmonize mwenyewe,Make Me Sing ya Aka na Diamond,Love Boat Kcee na.Diamond,Walk it off ya Fid Q na nyingine nyingi. 


Note:Wimbo wa BADO na interview ya Harmonize vimeambatanishwa kwenye barua pepe hii.