Monday, February 1, 2016

HII MPYA!!! PEP GUARDIOLA KUMRITHI MANUEL PELLEGRINI MWISHONI MWA MSIMU CITY!

Pep Guardiola ameteuliwa kuwa Meneja mpya Klabuni Manchester City kwa ajili ya Msimu ujao kwa Mkataba wa Miaka Mitatu.
Guardiola, Raia wa Spain mwenye Miaka 45 na ambae sasa ni Meneja wa Bayern Munich, atambadili Manuel Pellegrini ambae ataondoka Juni 30.
City wanajiandaa kukwaana na Sunderland mechi ijayo na tayari Pellegrini ameshatamka kwamba ukingo wake ni mwishoni mwa Msimu huu na Man City.
Taarifa kutoka Man City imesema Pellegrini, Raia wa Chile mwenye Miaka 62, ameafiki mabadiliko haya.
Pellegrini aliteuliwa kuwa Meneja wa City Mwaka 2013 na kuiongoza Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England na Kombe la Ligi Msimu uliofuatia.


KUHUSU PEP
PEP GUARDIOLA CAREER STATS
BARCELONA:
La Liga:
2008–09, 2009–10, 2010–11
Copa del Rey: 2008–09, 2011–12
Spanish Super Cup: 2009, 2010, 2011
Champions League: 2008–09, 2010–11
UEFA Super Cup: 2009, 2011
FIFA Club World Cup: 2009, 2011

BAYERN MUNICH:

Bundesliga: 2013–14, 2014–15
German Cup: 2013–14
UEFA Super Cup: 2013
FIFA Club World Cup: 2013


Meneja wa Manchester City Pellegrini akisherehekea Ubingwa wa 2014 wa Premier League huko Etihad Stadium

Pellegrini na Mwali wa  Capital One Cup walipoifunga  Sunderland huko Wembley  2014
Guardiola sasa kuchukuwa nafasi yake baada ya kujulikana leo Jumatatu kwa uhakika