Sunday, February 28, 2016

KAPOMBE MCHEZAJI BORA MWEZI JANUARI 2016


www.bukobasports.comBeki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2016. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting. Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari24, 2016. Kapombe alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 wa timu yake dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam kwenye mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare