Thursday, February 18, 2016

KUELEKEA KWENYE DABI YA JUMAMOSI: YANGA vs SIMBA, TIMU ZOTE MBILI ZATUA KIMYA KIMYA JIJINI DAR!

MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga wanatarajiwa kurejea Jijini Dar es Salaam hii Leo kwa Ndege ya kukodi na kwenda mafichoni kujiandaa na mchezo wake dhidi ya mahasimu wao wa jadi Simba utakaopigwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Jijini Dar es Salaam, Yanga watapiga kambi yake katika Hoteli moja ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano iliyopo katikati ya Jiji kwa ajili ya maandalizi yake ya mwisho kuelekea kwenye Dabi hiyo ya Kariakoo.
Wakati Yanga wakirejea leo Simba wenyewe wamerejea Dar jJana usiku wakitokea Mkoani Morogoro walipokuwa wameweka kambi katika Chuo cha Biblia.
Mara baada ya Timu hiyo kuwasil Kikosi kizima kilikutana na Viongozi kwa ajili ya kupewa maneno ya mwisho mwisho kuelekea kwenye pambano hilo ambapo walitakiwa kujituma na kuhakikisha wanaichapa Yanga kwenye pambano hilo.

Katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi, tayari Viongozi wa Simba wamewataka wanachama wa Matawi yao kuhakikisha Matawi yote kila moja linachanga kiasi cha pesa Shilingi laki tano kwa ajili ya kuwapa Wachezaji kama motisha ili waibuke na ushindi katika Dabi hii.

VPL-LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Februari 20

Yanga vs Simba
Mgambo JKT vs Tanzania Prisons
Stand United vs JKT Ruvu
Mbeya City vs Azam FC
Majimaji vs Mtibwa Sugar
Toto Africans vs Kagera Sugar

Jumapili Februari 21
Ndanda FC v African Sports
Mwadui FC v Coastal Union