Tuesday, February 9, 2016

KURT ZOUMA NJE MIEZI 6 CHELSEA

Beki wa klabu ya Chelsea Kurt Zouma atakua nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia goti kwenye mchezo dhidi ya Manchester United.
Zouma, atafanyiwa upasuaji kwenye kwenye goti lake ambalo aliumia Jumapili uwanjani Stamford Bridge baada ya kutua vibaya aliporuka kupiga mpira kwa kichwa.
Uchunguzi umethibitisha kwamba aliumia vibaya na hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kutibu tatizo hilo.
Kawaida, Mchezaji akipata majeruhi ya aina hii, basi huwa nje ya uwanja si chini ya Miezi hivyo mchezaji huyu atakosa michezo yote ya msimu uliobaki. Image copyright Reuters Image caption Zouma alionekana kuhisi uchungu mwingi baada ya kuanguka
Zouma, ambaye amekuwa kama pacha wa John Terry uwanjani, ameichezea Chelsea mechi 32 msimu huu.
Ameshaichezea Ufaransa mechi 2 za Kimataifa.