Tuesday, February 2, 2016

KUTUA GUARDIOLA MAN CITY, WADAU WAMWAGALIA VAN GAAL KUPINDULIWA NA JOSE MOURINHO KUTWAA MIKOBA OLD TRAFFORD!

Louis van Gaal atabadilishwa mwishoni mwa Msimu kwa mujibu wa ripoti toka huko England.
Gazeti la Daily Star la huko England limedai Mtendaji Mkuu wa Manchester United, Ed Woodward, ameshaamua sasa Van Gaal aondoke baada ya kuboronga Msimu huu.
Kwa mujibu wa Gazeti hilo, Man United itamchukua Jose Mourinho aliefukuzwa Chelsea ili kukabili changamoto ya Wapinzani wao wa jadi Man City kumteua Pep Guardiola kuwa Meneja mpya kwa ajili ya Msimu ujao.
Van Gaal, mwenye Miaka 64, bado ana Mwaka mmoja kwenye Mkataba wake baada ya Msimu huu kumalizika lakini mwenyewe alishatoa ofa ya kujiuzulu wakati wa Krismasi Timu ilipokuwa ikifanya vibaya.
Lakini, wakati huo, Man United ilikataa Van Gaal kujiuzulu na sasa hali ya Timu haina mabadiliko ila kuimarika kwa wapinzani wao ndiko kumeifanya Man United kutaka kumng'oa Van Gaal.
Kama ilivyo desturi Klabu ya Man United haijatamka lolote kuhusu ripoti hizi.