Saturday, February 6, 2016

KWA NINI MANCHESTER CITY WAMEFUNGWA 3-0 NA LEICESTER CITY?


Beki ya Man City ni dhaifu mno
Nicolas Otamendi alijikuta yupo chini baada ya kupigwa chenga hatari na Riyad Mahrez na kufunga, wakati Martin Demichelis alijikuta akishindwa kabisa kumdhibiti beki wa Leicester Robert Huth na kufunga magoli mawili kwa kichwa.
Kutokuwepo kwa Vincent Kompany ni pigo kubwa sana kwa Man City.
TOURE amechemka tena 

Utawala wa Toure sasa unaonekana kuisha Man City. Toure alijikuta akitolewa mapema kabisa katika kipindi cha pili.
Kimsingi hakuna namna Toure ataweza kubaki klabuni hapo wakati kocha mpya wa klabu hiyo Pep Guardiola atakapowasili.

MAHREZ ameidhalilisha safu ya ulinzi ya City.

Riyad Mahrez amekuwa ni mwiba mchungu kwa takriban kwa timu zote alizokutana nazo. Kwa maana hiyo Mahrez ni mchezaji asiyekabisa Uingereza kwa sasa. 
SCHMEICHEL ni moja ya makipa bora kwa sasa EPL

Pengine Mahrez na Jamie Vardy ndiyo wanaonekana kupewa pongezi kubwa sana kutokana na mwenendo mzuri wa Leicester msimy huu, lakini kipa wa klabu hiyo Kasper Schmeichel ni miongoni mwa watu muhimu wanaochangia matokeo mazuri ya timu hiyo. Leo aliokoa moja ya hatari kubwa sana kutoka kwa kiungo wa City Fernando.
RANIERI ni kocha mwenye kupandikiza ari kubwa kwa wachezaji wake

Hata wakati wakiwa wanaongo za kwa mabao 3-0, Ranieri bado alionekana kuwa na uchu na matokeo mazuri kwa timu yake na aliendelea kubaki akiwa amesimama huku akitoa maelekezo kwa wachezaji wake na kuwafanya wachezaji wake kuwa na ari ya hali ya juu.

Ubora wa viwango vya wachezaji kwa siku ya leo.
Man City: Hart 6, Zabaleta 4, Otamendi 3, Demichelis 3, Kolarov 4, Fernandinho 5, Delph 5 (Iheanacho 52, 4), Toure 3 (Fernando 52, 4), Sterling 5, Silva 4 (Celina 76, 5), Aguero 6

Leicester: Schmeichel 6, Simpson 6, Morgan 6, Huth 7, Fuchs 6, Kante 6, Drinkwater 7, Okazaki 6 (Ulloa 81, 4), Albrighton 6 (Dyer 86), Mahrez 8 (Gray 76, 4), Vardy 7

Mchezaji bora wa mchezo : Riyad Mahrez