Friday, February 12, 2016

LIGI KUU MZUNGUKO WA 19 KUENDELEA WIKIENDI HII.. JKT v KAGERA SUGAR, COASTAL UNION v AZAM FC USO KWA USO JUMAPILI!

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti, huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo. Jumamosi, Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Stand United watawakaribisha Simba SC, Mgambo Shooting v African Sports (Mkwakwani), Mbeya City v Toto Africans (Sokoine), Ndanda FC v Majimaji (Nangwanda) na JKT Ruvu v Kagera Sugar uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Mwadui FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mwadui Complex, huku Coastal Union wakicheza dhidi ya Azam FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.