Friday, February 26, 2016

LIVE: FIFA PRESIDENTIAL ELECTION


FIFA Acting President Issa Hayatou saw the organisation vote in favour of reforms to repair its image

Sheik Salman bin Ebrahim Al-Khalifa of Bahrain is a leading contender to be elected as FIFA presidentUchaguzi unaendelea mpaka sasa huko Zurich www.bukobasports.com
Shirikisho la soka duniani Fifa litampta kiongozi mpya leo wajumbe 207 watakapokusanyika mjini Zurich, Uswizi kumchagua mrithi wa Sepp Blatter.
Blatter, 79, aliongoza shirikisho hilo tangu 1998.
Aling’atuka mwaka jana kutokana na tuhuma za ufisadi zilizogubika shirikisho hilo.

Kuna wagombea watano wanaotaka kumrithi.
Watano hao ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne.
Sheikh Salman na Gianni Infantino ndio wanaopigiwa upatu kushinda.
Upigaji kura utaanza saa 12:00 GMT (saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki).
Kabla ya kura kupigwa, kila mgombea atakuwa na dakika 15 za kuhutubia wajumbe.
Kuna mataifa 209 wanachama wa FIFA lakini Kuwait na Indonesia kwa sasa hawashirikishwi, hivyo wajumbe watakaopiga kura ni 207.
Ili kutangazwa mshindi duru ya kwanza, mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa.
Hili lisipofanyika, wagombea wote wanapigiwa kura tena duru ya pili na anayepata kura nyingi kutangazwa mshindi.
Mshindi akikosekana duru ya pili, basi duru ya tatu hufanyika bila mgombea mwenye kura chache zaidi raundi ya pili.
Fifa imesema lazima mshindi ajulikane leo Ijumaa.