Thursday, February 25, 2016

FULL TIME: UEFA EUROPA LEAGUE, LIVERPOOL 1 v 0 AUGSBURG(Agg 1-0), JAMES MILNER AIWEKA LIVERPOOL NDANI YA 16 BORA!

PENATI ya Dakika ya 5 imewapa Liverpool ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Augsburg ya Germany Uwanjani Anfield katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Kwenye Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Germany Wiki iliyopita Timu hizi zilitoka Sare 0-0.
Penati hiyo ya Liverpool ilifungwa na James Milner na ilitolewa kwa madai kuwa Mchezaji wa Augsburg aliunawa Mpira.
Liverpool watamjua mpinzani wao kwenye Raundi inayofuata baada ya Droo itakayofanyika Ijumaa Februari 26 huko Nyon, Uswisi.
Klopp1-0James Milner aliipatia bao la kuongoza dakika ya 5 kwa mkwaju wa penatiVIKOSI:
Augsburg XI:
Hitz , Verhaegh, Janker, Klavan, Stafylidis, Kohr, Esswein, Koo, Altintop, Werner, Caiuby.
Subs: Manninger, Opare, Parker, Moravek, Bobadilla, Max, Rieder.

Liverpool XI: Mignolet, Clyne, Lucas, Sakho, Moreno, Can, Henderson, Milner, Firmino, Coutinho, Sturridge.
Subs: Ward, Toure, Benteke, Origi, Smith, Teixeira, Chirivella

LIVE: Liverpool vs Augsburg