Saturday, February 20, 2016

FULL TIME: YANGA 2 v 0 SIMBA, DONALD NGOMA NA TAMBWE WAICHAPA SIMBA TAIFA LEO!

MABINGWA Watetezi wa VPL, LIGI KUU VODACOM , Yanga, Leo wameidunda Simba 2-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kurejea kileleni mwa Ligi.
Refa Mwanamama, Jonesia Rukya, aliipa pigo Simba kwa kumtoa nje Abdi Banda baada ya kupewa Kadi za Njano 2 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 24.
Straika kutoka Zimbabwe, Donal Ngoma, aliipa Yanga Bao la kwanza Dakika ya 40 pale Beki wa Simba, Hassan Kessy alipotoa pasi kumrudishia Kipa Vincent Angban na Ngoma kuinasa pasi hiyo na kumzunguka Kipa na kufunga.

Kipindi cha Pili Dakika ya 73, Mchezaji wa Burundi, Amisi Tambwe, aliihakikishia Yanga ushindi mnono alipounganisha Krosi ya na kutikisa Nyavu.

Hii ni mara ya pili kwa Yanga kuibamiza Simba 2-0 katika VPL Msimu huu ambapo Mwezi Septemba walishinda Mechi ya kwanza ya Ligi.

Huko Sokoine, Mbeya Azam FC wameitwanga Mbeya City Bao 3-0 kwa Bao za Kipre Herman Tchetche, John Raphael Bocco na Farid Mussa na kukamata Nafasi ya Pili ya VPL.