Sunday, February 7, 2016

FULL TIME: CHELSEA 1 v 1 MANCHESTER UNITED, DIEGO COSTA AIOKOA BLUES DARAJANI DAKIKA ZA LALA SALAMA!

Diego Costa akishangilia bao lake la kusawazishaTerry nae aliunga mkono kugawana pointi katika sare hiyo
Diego Costa alipowasawazishia bao Chelsea dakika za lala salama kwa kufanya 1-1
Mabingwa wa England, Chelsea, hii Leo wamefanikiwa kupata Sare Uwanjani kwao Stamford Bridge baada ya kusawazisha Dakika za Majeruhi na kuambua Sare ya 1-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Sare hii inaibakisha kila Timu Nafasi yake ile ile, Man United ikiwa ya 5 na Chelsea ya 13 na kuondoa matumaini kwao kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa Msimu huu na pengine kufuta matumaini ya Chelsea kucheza Ulaya Msimu huu huku Man United, walio Pointi 6 nyuma ya Timu ya 4 Man City wakiwa bado na matumaini ya kuwepo Ulaya Msimu ujao.Jesse Lingard aliipa Man United Bao la kuongoza Dakika ya 61 kufuatia Krosi ya Cameron Borthwick-Jackson ambayo ilimkuta Wayne Rooney kumsogezea Lingard.
Chelsea walisawazisha Dakika ya 91 kwa Bao la Diego Costa.

Jumamosi ijayo Man United wako Ugenini huko Stadium of Light kucheza na Sunderland wakati Chelsea wako kwao Stamford Bridge kupiga na Newcastle.
Lingard alivyoifungia bao Man United kipindi cha pili1-0
Chelsea na Man United wakutana Tena leo, Nani kuibuka Bingwa mara ya mwisho walitoka 0-0