Saturday, February 6, 2016

FULL TIME: MANCHESTER CITY 1 v 3 LEICESTER CITY, ROBERT HURT, RIYAD MAHREZ WAICHINJA CITY ETIHAD LEO!! SASA WAKO POINTI 6 KILELENI!

Robert Hurt anaimaliza tena kwa bao lake la pili la kichwa dakika ya 60 kwa kuifungia Leicester bao la tatu na kufanya 3-0 dhidi ya Wenyeji Timu ya Manchester City. Sergio Ag├╝ero Dakika ya 87 aliwafungia bao la kufutia machozi City na kufanya matokeo kuwa 3-1Kipindi cha pili dakika 48 Riyad Mahrez aliwachambua mabeki wa City na kuwafunga  bao la pili na kufanya bao kuwa 2-0.Leicester washikilia uongozi sasa!! Kipa wa City Hart akipagawa baada ya kufungwa bao ndani ya muda mchache Etihad. Kipindi cha kwanza kinamalizika City wako nyuma  0-1 Leicester 1-0Robert Hurt tayari kawaamusha Mashabiki kwenye Viti Etihad kwa kuifungia bao la haraka Leicester CityRobert Huth dakika ya 3 anaipachikia bao la kuongoza Leicester City wakicha kwenye Uwanja wa Etihad Stadium.