Monday, February 22, 2016

FULL TIME: SHREWSBURY 0 vs 3 MANCHESTER UNITED, CHRIS SMALLING, JUAN MATA NA LINGARD WAIPELEKA ROBO FAINALI UNITED, SASA KUKUTANA NA WEST HAM OLD TRAFFORD!

Ndani ya Uwanja wa Greenhous Meadow, Manchester United waliisambaratisha Timu ya Daraja la chini la Ligi 1, Shrewsbury Town, katika Mechi ya mwisho ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP Bao 3-0 na kutinga Raundi ya 6 ambayo ni Robo Fainali ambapo watakutana na West Ham huko Old Trafford.
Bao za Kipindi cha Kwanza za Dakika za 37 kupitia Chris Smalling na Frikiki ya Juan Mata ya Dakika ya 45 ziliwapa Man United uongozi wa 2-0 hadi Mapumziko.
Jesse Lingard alipiga Bao la 3 Dakika ya 61 na kuwapa Man United ushindi wa raha wa 3-0 ambao umeondoa presha kwa Meneja wao, Luis van Gaal, anaesakamwa hasa baada ya kufungwa Mechi 2 mfululizo zilizopita dhidi ya Sunderland, kwenye Ligi Kuu England, na toka kwa FC Midtjylland huko Denmark kwenye UEFA EUROPA LIGI.
Alhamisi, Man United wako kwao Old Trafford kurudiana na FC Midtjylland wakitakiwa kupindua ushindi wa Wadenishi hao wa Bao 2-1.Van Gaal na GiggsFriikiki ya Juan Mata dakika ya 45 imewapa bao jingine la pili na kuifanya United kwenda mapumziko ikiwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya timu ya Shrewsbury. Kipindi cha pili dakika ya 62 Lingard kafanikisha 3-0Chris Smalling kafanikisha bao la kwanza kwa Man united kwa kufanya 1-0 dakika ya 37 kipindi cha kwanza0-0Van GaalVIKOSI:
Shrewsbury:
Leutwiler, Whitbread, Grandison, Black, Whalley, Brown, Grimmer, Ogogo, Mangan, Knight-Percival, Akpa Akpro.
AKIBA: Halstead, Sadler, Vernon, Clark, Cole, Smith, Grandin.

Manchester United: Romero, Varela, Smalling, Blind, Borthwick-Jackson, Schneiderlin, Herrera, Memphis, Mata, Lingard, Martial. 

AKIBA: Henderson, McNair, Poole, Carrick, Pereira, Riley, Keane.
Refa: Robert Madley


Michael Carrick akisonga kwenye Uwanja wa  Greenhous Meadow punde kabla ya kipute kuanzaJuan Mata