Sunday, February 21, 2016

SPANISH PRIMERA DIVISIÓN: MALAGA 1 v 1 REAL MADRID, RAUL ALBENTOSA AONGOZA MALAGA KUIBANA REAL TENA LEO!

Real Madrid Leo wameshindwa kupunguza pengo lao na Vinara wa La Liga Barcelona baada ya kubanwa na kutoka Sare ya 1-1 ugenini na Malaga.
Real walitangulia kufunga Dakika ya 37 kwa Bao la Cristiano Ronaldo lakini Malaga, waliocheza vizuri sana Mechi hii, wakasawazisha Dakika ya 67 kwa Bao la Albentosa. Mbele ya Meneja Zinedine Zidane
Barcelona bado wako kileleni wakiwa na Pointi 63 wakifuata Real na Atletico wote wakifungana kwa Pointi 54 lakini Usiku huu Atletico, waliocheza Mechi 1 pungufu, wapo Nyumbani kucheza na Villareal na wanaweza wakaounguza pengo na Barca na pia kuitambuka Real na kukamata Nafasi ya Pili.MSIMAMO