Saturday, February 13, 2016

FULL TIME: SUNDERLAND 2 v 1 MANCHESTER UNITED

David De Gea kajifunga bao dakika ya 82 na kuwapa bao la pili Sunderland kwa kufanya 2-1.
Sunderland walitangulia kupata Bao Dakika ya 3 tu baada ya Frikiki ya Wahbi Khazri kupenya chini na kumshinda Kipa David de Gea.
Man United walisawazisha Dakika ya 39 kufuatia Shuti la Juan Mata kutemwa na Kipa Mannone na kumfikia Anthoby Martial aliefunga kifundi.
Bao hizo zilidumu hadi Mapumziko.
Sunderland walifunga Bao lao la pili Dakika ya 82 kwa Kichwa cha Lamine Kone baada ya Mpira wa Kona kuokolewa mstarini na Martial na kumgonga Kipa De Gea na kutinga.
Hadi mwisho Sunderland 2 Man United 1.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika Timu zote zilienda mapumziko zikiwa sare ya 1-1. Man United wakisawazishiwa bao lao na Mchezaji wake matata Anthony Martial dakika ya 39.1-0Mchezaji mpya wa Sunderland Wahbi Khazri aliipatia bao la kwanza na kuipatia bao la kuongoza 1-0 dhidi ya Man United kwa mpira wa adhabu(friikiki) dakika ya 3 tu ya mchezo.Wakifanya mazoezi kabla ya mtanange kuanza punde.
VIKOSI:
Sunderland:
Mannone, Yedlin, O’Shea, Kone, van Aanholt, Kirchhoff, Cattermole, M’Vila, Khazri, N’Doye, Defoe
Akiba: Brown, Rodwell, Borini, Matthews, Pickford, Toivonen, Honeyman
Manchester United: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, Borthwick-Jackson, Schneiderlin, Carrick, Lingard, Mata, Martial, Rooney
Akiba: Romero, Love, Weir, Pereira, Herrera, Depay, Keane