Friday, February 5, 2016

LOUIS VAN GAAL ASEMA MBIO ZA UBINGWA MSIMU 2015/2016 BADO WANAZINYEMELEA MAN UNITED!

Van Gaal anaamini Kikosi chake kikiipiga Timu ya Chelsea Jumapili Februari 7, 2016 Klabu hiyo ya Mashetani wekundu itakuwa inapigania vyema Ubingwa huo wa Msimu huu wa 2015/16. Mpaka sasa Man United ipo nyuma ya pointi 10 na timu ya Leicester City yenye Alama 50 na Man United 40. Mchezo huo wa Blues na United utakaopigwa jumapili 7 saa 1:00 usiku utakuw ni wa ushindani mkubwa kwani pia hata Chelsea wanajikwamua kutoka chini ili waingie top 4 huku Man United ikifukuzia ubingwa msimu huu.
Louis van Gaal anaamini Manchester United ipo kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu England hasa baada ya kuonyesha Soka safi katika Mechi zao 2 zilizopita.
Msimu huu, Meneja Van Gaal amekuwa akisakamwa sana baada ya Timu yake kucheza Soka la ovyo na kutokuwa na mtiririko mzuri wa ushindi.
Lakini Van Gaal anaamini ikiwa Man United itaifunga Chelsea huko Stamford Bridge Jumapili itakuwa imerudi kwenye reli kugombea Ubingwa.
Man United wapo Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya 4 Arsenal na Pointi 10 nyuma ya Vinara Leicester City.
Hivi sasa Man United imepoteza Mechi 1 tu kati ya 8 ilizocheza mwisho na baada ya kuichapa Derby County 3-1 kwenye FA CUP na kisha kuitwanga Stoke City 3-0 kwenye Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford Jumanne iliyopita, Timu inaelekea kupata mwelekeo mpya wa ushindi.
Akiongea na Wanahabari hii Leo, Van Gaal alisema: “Hatukuzi mambo ila nina hisia tutaifunga Chelsea ingawa hilo ni gumu kwa vile chini ya Guus Hiddink hawafungwi. Tukishinda, Ligi yetu inaanza!”
Aliongeza: “Siku zote nimesema ni Mechi za Crystal Palace na Arsenal pekee ambazo Timu hizo zilionekana bora kupita Manchester United, nyingine zote sisi tulikuwa juu!”

Man United watatinga kucheza na Chelsea, ambao wako Nafasi ya 13, bila ya Majeruhi Bastian Schweinsteiger, Ashley Young, Marcos Rojo, Luke Shaw na Antonio Valencia.

Tangu wamtimue Jose Mourinho Mwezi Desemba, Chelsea, chini ya Meneja wa muda Guus Hiddink, haijapoteza Mechi yeyote katika Mechi zao 8 na ilitoka 0-0 na Man United Uwanjani Old Trafford Desemba 28 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu.


Vikosi vinaweza kuwa hivi jumapili keso kutwa