Sunday, February 28, 2016

MAN UNITED 3 - 2 ARSENAL, MATUMAINI YA UBINGWA ARSENAL YAANZA KUYEYUSHWA OLD TRAFFORD. RASHFORD NA HERRERA WAKIINYUKA GUNNERS!

Rashford nae amepaa kushangilia na wenzakeMashabi wakimpongeza Rashford baada ya kutoka kwa kupumzishwa!


Shangwe!
Manchester United, Leo Old Trafford ikicheza na‘Kikosi cha kungaunga’, iliibamiza Arsenal Bao 3-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kutia doa kubwa nia yao kutwaa Ubingwa. 
Hakuna alietegemea Kikosi cha Man United bila Kepteni Wayne Rooney, Chris Smalling, Anthony Martial, Antonia Valencia, Ashley Young, Phil Jones, Luke Shaw, na kikiwa na Makinda Varela, Lingard, Memphis na zaidi, toto dogo, Marcus Rashford, huku Sentahafu ni Kiungo Michael Carrick, kinaweza kuisimamisha Arsenal inayotegemewa kuwa Mabingwa Msimu huu.

Lakini hilo Chipukizi wa Miaka 18, Marcus Rashford, hakulijua na akabamiza Bao 2 kwa mara ya kwanza katika Ligi na kuwa Dogo mdogo kabisa wa kwanza kufunga Bao za Ligi katika Historia ya Man United na kuendeleza wimbi lake la Mabao tangu aanze kukichezea Kikosi cha Kwanza cha Man United Juzi Alhamisi alipoiga Bao 2 wakati Timu yake inaibamiza FC Midtjylland Bao 5-1 katika UEFA EUROPA LIGI.
Bao la 3 la Man United lilifungwa na Ander Herrera.
Bao za Arsenal zilipigwa na Danny Welbeck na Mesut Ozil.
Van Gaal leo kaonesha mbwembwe mbele ya Umati wa Mashabiki 75, 326Van Gaal chini akimwonesha Mwamuzi kile ambacho kakiona uwanjani kwamba si sawa!Van Gaal akionesha makeke!Nini!! Mnawabeba??