Wednesday, February 17, 2016

MAYANJA: KWA MFUMO WAO, YANGA NITAWAPIGA HATA 3-0

Na Princess Asia, MOROGOROKOCHA Mganda wa Simba SC, Jackson Mayanja (pichani) amesema kwa mfumo wanaotumia Yanga SC anaweza kuwafunga hata mabao 3-0 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Uganda, aliyejiunga na Simba SC katikati ya Januari baada ya kuondolewa kwa Muingereza, Dylan Kerr amesema kwamba amekuwa akiifuatilia Yanga inayofundishwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm kwa muda mrefu, hususan kwenye michezo yao mitano iliyopita ya Ligi Kuu na haoni kwa nini asiwafunge Jumamosi.