Friday, February 12, 2016

MESSI NDIYE MCHEZAJI BORA WA MWEZI SPAIN

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ndiye mchezaji bora mwezi huu nchini Uhispania ,ikiwa ni mara ya kwanza kushinda taji hilo.
Tuzo hiyo ilitolewa msimu wa 2013-2013 ,lakini Messi ambaye ni mchezaji bora dunia mara tano alikuwa hajashinda tuzo katika mara 22 ambalo lilitolewa.
Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 28,hatimaye ametuzwa baada ya kufunga mabao matano katika mechi sita alizocheza mnamo mwezi Januari.
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda taji hilo mara mbili tangu lianzishwe mnamo mwezi Septemba 2013.
Wachezaji wa Atletico Madrid Diego Godin na Antoine Griezman,pamoja na mshambuliaji wa Real Sociadad Carlos Vela pia wameshinda mara mbili.

Messi ni mchezaji wa pili katika kilabu ya Barcelona kushinda taji hilo baada ya Neymar mnamo mwezi Novemba.