Sunday, February 7, 2016

MOURINHO AFUNGUKA, ASEMA ATABANANA PALE PALE ENGLAND, ASEMA...KIBARUA KINACHOFUATA NI ENGLAND!

Jose Mourinho amedokeza kuwa kazi yake ijayo itakuwa kwenye Ligi Kuu England na yupo tayari kuendelea kuwa Meneja wa Klabu ya Soka.
Mreno huyo amehusishwa na Klabu kadhaa huko Ulaya tangu atimuliwe Chelsea Mwezi Desemba.
Katika Siku mbili hizi kumeibuka habari kuwa Wawakilishi wapo mazungumzoni na Manchester United.
Akiongea kwa mara ya kwanza kwenye Mahojiano na Kituo cha TV tangu aondoke Chelsea, Mourinho ametoboa kuwa anataka kubakia England na Familia yake.
Amesema: "Sasa hivi sina kazi lakini London ndio Nyumbani kwetu."

Mourinho alirudi Chelsea kwa mara ya pili na kuiwezesha Chelsea kutwaa Ubingwa Msimu uliopita lakini Msimu huu ilianza vibaya na kutupwa Nafasi ya 16 wakati alipotimuliwa.
Mbali ya Vipindi vyake viwili na Chelsea, Mourinho pia kuongoza Klabu huko kwao Portugal, Italy na Spain ambako alikuwa na Real Madrid.
Kuhusu kurejea tena Spain, Mourinho amesema hawezi kurejea huko kwa sababu ushindani ni hafifu.
Ameeleza: "Siku zote napenda ushindani. Nataka ushindani wa kila Wiki na huko Spain nilikuwa kwenye Klabu lakini Mechi za ushindani zilikuwa 4 tu kwa Mwaka: Barcelona v Real Madrid, Real Madrid v Barcelona na baada ya hapo tunashinda 4-0, 5-0, 4-1, 6-1,"

Aliongeza: "Nilikuwa Bingwa nikiwa na Pointi 100 lakini niliukosa nikiwa na Pointi 91! Hapa England unaweza kutwaa Ubingwa ukiwa na Pointi 75 au chache. Hivyo nahitaji ushindani!"