Saturday, February 13, 2016

MVUA YA MAGOLI!! 8-0 NA 7-0 ZA LEO, TFF YASITISHA KUTANGAZA TIMU ILIYOPANDA LIGI KUU MPAKA!!

www.bukobasports.comTFF HAITATANGAZA MSHINDI WA STARTIMES KUNDI C
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitatangaza timu iliyopanda Ligi Kuu msimu ujao kutoka Kundi C, mpaka itakapoamuliwa na vyombo husika vya TFF baada ya michezo ya kundi hilo kuchezwa leo jioni katika viwanja tofauti nchini.
TFF imefikia hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za michezo kati ya JKT Kanembwa v Geita Gold na Polisi Tabora v JKT Oljoro iliyochezwa leo jioni katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
Taarifa za michezo hiyo kutoka kwa wasimamizi husika na vyanzo vingine vinakusanywa ili zifanyiwe kazi na vyombo husika vya TFF.

Katika michezo hiyo ya leo, Geita iliibuka na ushindi wa mbao 8 – 0 dhidi ya JKT Kanembwa, huku Polisi Tabora wakiibuka na ushindi wa mabao 7 – 0 dhidi ya JKT Oljoro.

IMETOLEWA NA TFF
Matokeo:
Jumamosi Februari 13
Kundi B

Kimondo FC 2 Kurugenzi FC 0
Njombe Mji 2 Lipuli FC 0
Ruvu Shooting 0 Polisi Morogoro 0
Burkinafaso FC 2 JKT Mlale 3

Kundi C

Mbao FC 1 Polisi Mara 1
Polisi Tabora 7 JKT Oljoro 0
JKT Kanembwa 0 Geita Gold FC 8