Monday, February 29, 2016

RATIBA LIGI KUU ENGLAND KUPIGWA KATIKATI YA WIKI, JUMANNE NA JUMATANO - LIVERPOOL v MANCHESTER CITY KURUDIANA

Ligi Kuu England dimbani Jumanne na Jumatano Usiku kwa Timu zote 20 kushuka Uwanjani ambapo Vinara Leicester City Jumanne watakuwa kwao kucheza na West Bromwich Albion.
Mbali ya Mechi hiyo Jumanne zipo Mechi nyingine 4 ambapo pia Mabingwa Watetezi Chelsea watacheza wakiwa Ugenini na Norwich City.
Jumatano pia zipo Mechi 5 na Timu ya Nafasi ya Pili Tottenham itacheza Ugenini katika Dabi ya Jiji la London huko Upton Park na West Ham wakati Timu ya 3, Arsenal, ikiwa Nyumbani kucheza na Swansea City.
Mtanange mkali uko huko Anfield ambapo Liverpool itacheza na Man City ikiwa ni mara pili kukutana ndani ya Siku 3 baada ya Jumapili kucheza Fainali ya Capital One Cup huko Wembley Jijini London na City kutwaa Kombe kwa Penati 3-1 kufuatia Sare ya 1-1 katika Dakika 120 za Gemu.
Mechi nyingine ni ile ambayo iko Old Trafford wakati Man United, wakitoka tu kuitwanga Arsenal 3-2 Jumapili, watacheza na Watford United.
Man United wapo Nafasi ya 5.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumanne Machi 1
{Mechi zote  22:45}

Aston Villa v Everton
Bournemouth v Southampton
Leicester v West Brom
Norwich v Chelsea
Sunderland v Crystal Palace
Jumatano Machi 2
22:45 Arsenal v Swansea
22:45 Stoke v Newcastle
22:45 West Ham v Tottenham
23:00 Liverpool v Man City
23:00 Man United v Watford

Jumamosi Machi 5
15:45 Tottenham c Arsenal
{Mechi zote kuanza Saa 18:00}
Southampton v Sunderland
Man City v Aston Villa
Chelsea v Stoke City
Everton v West Ham
Swansea City v Norwich City
Newcastle v Bournemouth
Watford v Leicester City

Jumapili Machi 6

16:30 Crystal Palace v Liverpool
19:00 West Brom v Man United