Sunday, February 14, 2016

RATIBA UEFA CHAMPIONS, JUMANNE NA JUMATANO KUPIGWA.. PSG V CHELSEA, JUMATANO NI AS ROMA v REAL MADRID

UEFA CHAMPIONS LIGI, inarejea tena kuanzia Jumanne Usiku kwa Mechi 2 za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Raundi hii inafuatia kumalizika kwa Mechi za Makundi Mwezi Desemba na Timu 16 kusonga.
Jumanne Benfica ya Portugal iko kwao kucheza na Klabu ya Urusi Zenit Saint Petersburg na Paris St Germaine itakuwa Nyumbani Jijini Paris Nchini France kuwavaa Mabingwa wa England Chelsea.

Siku ya Pili, Jumatano, zipo Mechi mbili pia kwa KAA Gent ya Belgium kuwa Nyumbani kucheza na Wajerumani VfL Wolfsburg wakati AS Roma ya Italy wako kwao kupambana na Vigogo wa Spain Real Madrid.
Mechi nyingine za kwanza za UCL za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitachezwa Jumanne na Jumatano Februari 23 na 24. 


UEFA CHAMPIONS LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
JUMANNE 16 FEB 2016

Benfica vs Zenit Saint Petersburg
Paris St Germaine vs Chelsea

JUMATANO 17 FEB 2016
KAA Gent v VfL Wolfsburg
AS Roma v Real Madrid 


UEFA CHAMPIONS LIGI

RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Mechi zote  Saa 4 Dakika 45 Usiku
JUMANNE 23 FEB 2016

Arsenal v Barcelona
Juventus v Bayern Munich

JUMATANO 24 FEB 2016

Dynamo Kiev vs Man City
PSV Eindhoven vs Atletico Madrid

Marudiano
JUMANNE 8 MAR 2016

Real Madrid vs AS Roma
VfL Wolfsburg vs KAA Gent

JUMATANO 9 MAR 2016
20:00 Zenit St Petersburg vs Benfica
Chelsea vs Paris St Germaine

JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico Madrid vs PSV Eindhoven
Man City vs Dynamo Kiev

JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v Arsenal
Bayern Munich v Juventus

TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:

-Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16: Desemba 14
Mechi Februari 16/17/23/24 na Marudiano Machi 8/9/15/16
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4

FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy