Wednesday, February 10, 2016

RATIBA YA UEFA CHAMPIONS LIGI: KLABU ZATAKA MABADILIKO!

CHAMA cha Klabu za Soka Ulaya, European Clubs' Association (ECA), kimesema kinataka mabadiliko kwenye Mfumo wa Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, lakini kimepuuza dhana kuwa wanataka kuanzisha ‘Supa Ligi ya Klabu za Ulaya’.
ECA imesema itafanya kazi na UEFA ili kuboresha UCL kabla ya Mwaka 2018.
Mwenyekiti wa ECA, Karl-Heinz Rummenigge, amehusishwa na kuanzisha kwa ‘Supa Ligi’ itakayokuwa Timu 20 kutoka Nchi za Italy, England, Spain, Germany na France.
Kwa mfumo wa sasa wa UCL, Klabu 78 hufuzu kucheza kutoka Nchi 54 Wanachama wa UEFA na baada ya Raundi za awali za mtoano, Timu 32 huingia hatua ya Makundi.
Kufuatia Kikao chao cha Jana, ECA kimesema kinafanyia kazi kutoa mapendekezo yao.
Wanachama wa ECA ni Zaidi ya Klabu 200 Barani Ulaya wakiwemo Vigogo Real Madrid, Barcelona, Juventus, Bayern Munich, Manchester United na Chelsea.
Mabadiliko kwenye Mfumo wa UCL huwezi kufanyika kila baada ya Miaka Mitatu na Miaka Mitatu ya sasa itakwisha baada ya Msimu wa 2017/18 kumalizika.
UEFA CHAMPIONS LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16

Mechi zote  Saa 4 Dakika 45 Usiku
JUMANNE 16 FEB 2016
Benfica v Zenit Saint Petrsburg
Paris St Germaine v Chelsea

JUMATANO 17 FEB 2016
KAA Gent v VfL Wolfsburg
AS Roma v Real Madrid

JUMANNE 23 FEB 2016
Arsenal v Barcelona
Juventus v Bayern Munich

JUMATANO 24 FEB 2016
Dynamo Kiev v Man City
PSV Eindhoven v Atletico Madrid

Marudiano
JUMANNE 8 MAR 2016

Real Madrid v AS Roma
VfL Wolfsburg v KAA Gent

JUMATANO 9 MAR 2016
2000 Zenit St Petersburg v Benfica
Chelsea v Paris St Germaine

JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico Madrid v PSV Eindhoven
Man City v Dynamo Kiev

JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v Arsenal
Bayern Munich v Juventus