Saturday, February 27, 2016

SHEREHE YA KIPINDI CHA SPORTS HEADQUATERS KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA MAPINDUZI YA MICHEZO.


Pichani Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata keki ya birthday ya kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake.

Efm 93.7 Radio kupitia kipindi chake cha Sports headquarters kimesheherekea kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake February 2015, hafla hiyo ilifanyika pale City Sports Lounge na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo akiwemo Waziri wa Habari, utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kama mgeni rasmi. Nikipindi pekee kilicholeta mapinduzi zaidi ya michezo kwa utangazaji na uchambuzi yakinifu nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa EfmRadio Frances Ciza akimlisha keki mgeni rasmi wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa na watendaji wa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Headquarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake

Watendaji wa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Headquarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio wakiserebuka kwa furaha City Sports Lounge jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Simba SC Haji Manara akimsikiliza Afisa habari wa TFF, Baraka Kiziguto akihutubia kwenye hafla hiyo