Saturday, February 27, 2016

SHULE YA WASICHANA YA JOSIAH BUKOBA WAFANYA IBADA YA SHUKRANI SHULENI KWAO LEO

Mkuu wa Shule amewapongeza sana Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2015 na kwa Ufaulu mzuri. Pia amewamwagia sifa kemkem Walimu kwa ujumla huku akipongeza Wazazi, uongozi wa shule hiyo kwa kufanikisha siku hii ya leo kwa kumshukuru Mungu kwani amejibu Sala zao na kuwawezesha wote kufaulu vizuri mtihani wao wa Taifa. Mwaka 2015 Wanafunzi 47 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Taifa kidato cha Nne, Wanafunzi 36 wamefaulu kwa Daraja la kwanza na Wanafunzi 11 wamefaulu kwa daraja la pili. Katika matokeo haya Shule imekuwa ya 2 kati ya shule 192 Kimkoa na ya 17 kati ya Shule 3452 Kitaifa. Aidha , wanampongeza Mkuu wa Shule, Mkurugenzi na Uongozi mzima kwa uwezeshaji mkubwa sana hadi kufikia mafanikio hayo.

Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba Abedinego Kesho mshahara ndiye aliyeongoza Ibada Shuleni hapo leo.Wa pili (kulia) ni Mkuu wa Shule Josia Girls High Schoolakiwa sambamba na Viongozi wa shule Hiyo
Baadhi ya Walimu wa Shule hiyo wakifuatilia kwa karibu Ibada


Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba Abedinego Kesho mshahara akiendesha Ibada ya shukrani.
Wanafunzi wakiimba Wimbo wa Kwaya ya RC Josiah SS wakati wa Ibada ya Shukrani leo hii jumamosi
Baadhi ya Wanafunzi wa Josiah wakifuatilia kwa karibu Ibada hiyo
Mwenyekiti wa bodi ya shule, Johansen Rutabingwa akiongea wakati wa Ibada hiyo

Wakimpongeza Mwanafunzi aliyefanya vizuri sana kwenye Mtihani wa kidato cha Nne kwa kupata Daraja la 1
Pongezi
Picha ya Pamoja baadhi ya Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na Viongozi wa Dini

Picha ya pamoja wahitimu wa kidato cha Nne, Walimu pamoja Viongozi wa Dini

Wanafuzi wakiwa kwenye picha ya pamoja
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu kidato cha NNE 2015 na kufanya vizuri kwenye Mitihani yao ambapo 36 walifaulu daraja la kwanza na wanafunzi 11 wamepata daraja la pili.