Friday, February 5, 2016

SWALI JUU YA SWALI! LEICESTER WATAWEZA KUIFUNGA MANCHESTER CITY?

Ligi kuu ya soka ya England inatarajiwa kuendelea tena Jumamosi kwa michezo mbalimbali katika viwanja tofauti, Manchester City watakuwa wenyeji wa Leicester, Aston Villa watamenyana na Norwich city, Liverpool watawaalika Sunderland, Newcastle united dhidi ya West Brom, Stoke watakuwa wenyeji wa Everton,Swansea watawakabili Crystal Palace, Watford watakuwa wageni wa Tottenham, na Southampton watakuwa nyumbani dhidi ya West Ham.