Monday, February 22, 2016

TIMU YA SOKA YA SINGIDA UNITED YAPANDA DARAJA


Na Jumbe Ismailly, Singida
TIMU ya soka ya Singida United ya mjini Singida hatimaye imekata tiketi ya kucheza ligi daraja la kwanza mwaka huu baada ya kuifunga bila huruma timu ya Abajalo F.C. ya wilayani Igunga,Mkoani Tabora kwa jumla ya magoli 2-0.

Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya michezo wa Namfua mjini Singida na kuhudhuriwa na wapenzi na washabiki wa soka wachache. Inadaiwa kuwa mchezo huo uliokuwa na mahudhurio hafifu kwa kiasi kikubwa yaliathirika na mchezo kati ya Yanga na Simba za jijini Dar-es-salaam.