Friday, February 26, 2016

TOKYO SEXWALE AJIONDOA UCHAGUZI WA URAIS FIFA.

Mgombea wa urais wa Fifa kutoka Afrika Tokyo Sexwale kutoka Afrika Kusini amejiondoa kutoka kwenye uchaguzi wa kuchagua mrithi wa Sepp Blatter.
Bw Sexwale, akihutubu kabla ya kura kupigwa, amesema hataki kugawanya kura na akawahimiza wajumbe waamue kati ya wagombea wanne waliosalia.
Ameahidi kuunga mkono na kufanya kazi na atakayeshinda.
"Nafikisha kampeni yangu kikomo hapa," amesema.
Wagombea waliosalia ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, na Jerome Champagne.