Tuesday, February 16, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE LEO JUMANNE PSG v CHELSEA: JOHN TERRY NJE, OSCAR NDANI KUELEKEA PARIS, IBRA AWASUBIRI KWA HAMU!

JOHN TERRY hayumo kwenye Kikosi cha Chelsea kilichoruka Mchana wa Leo kuelekea Paris, France ambako Kesho Jumanne Usiku watatinga ndani ya Parc des Princes kucheza na Paris Saint-Germain katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL.
Licha ya Leo Terry kufanya Mazoezi na wenzake Jijini London, Sentahafu hakuwemo kwenye Timu iliyopanda Ndege kwenda Paris kutokana nab ado kusumbuliwa na maumivu ya Musuli za Pajani aliyopata kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita.Kwenye Mechi hiyo ambayo Chelsea waliibamiza Newcastle 5-1, Terry, mwenye Miaka 35, alitolewa Kipindi cha Kwanza na Nafasi yake kuchukuliwa na Baba Rahman.
Pengo hili linaweza kumfanya Meneja wa Chelsea, Guus Hiddink, kumuanzisha Baba Rahman Fulbeki ya Kushoto na Branislav Ivanovic kuchukua nafasi ya Terry kwenye Sentahafu huku Cesar Azpilicueta akicheza kama Fulbeki wa Kushoto.

Eden Hazard

Pedro

Cesar Azpilicueta karibu na  Cesc Fabregas