Thursday, February 4, 2016

VPL: NDANDA FC YAIFUNZA COASTAL TANGA, MBEYA CITY 2-1 JKT RUVU

www.bukobasports.com
LIGI KUU VODACOM
MATOKEO
Alhamisi Februari 4

Coastal Union 0 vs 1 Ndanda FC
JKT Ruvu 1 vs 2 Mbeya City

--------------------------
LEO zilikuwepo Mechi 2 za Ligi Kuu Vodacom, VPL, huko Tanga na Jijini Dar es Salaam ambako Timu Ngeni ndizo ziliibuka Washindi.
Huko Mkwakwani, Tanga, Ndanda FC iliwatungua Wenyeji Coastal Union Bao 1-0 huku
Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Karume, Mbeya City walitangulia kufunga Dakika ya 23 kwa Bao la Hassan Mwasapili na JKT Ruvu kusawazisha Dakika ya 38 Mfungaji akiwa Mussa Juma lakini Dakika ya 45 Yohana Morris akaipa Mbeya City Bao la Pili na la ushindi wa 2-1.

LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Februari 6

Kagera Sugar vs Simba
African Sports vs Stand United

Jumapili Februari 7
Mbeya City vs Tanzania Prisons
JKT Ruvu vs Yanga
Ndanda FC vs Mtibwa Sugar
Azam FC vs Mwadui FC
Toto Africans vs Coastal Union
Majimaji vs Mgambo JKT