Wednesday, February 3, 2016

FULL TIME: TANZANIA PRISON 2 v 2 YANGA, SIMON MSUVA AIOKOA YANGA MBEYA KWA KUTOKA SARE!

Dakika ya 84 Yanga wanapata penati na kufungwa na Simoni Msuva na kuisawazishia Yanga bao kwa kufanya 2-2. Hilo bao ni la 4 kwa Msuva msimu huu. 
Sare hii inawaweka Yanga kileleni kwa pointi 40.

Dakika ya 62 Mohamed Mkopi mchezaji wa zamani wa Timu ya Mtibwa Sugar anaipachikia bao la pili na kufanya Tanzania Prisons kuongoza kwa bao 2-1 dhidi ya Yanga ya Jijini Dar es Saalam.

Jeremiah Juma dakika ya 40 anaisawazishia bao Tanzania Prisons na kufanya 1-1 katika kipindi cha kwanza. Bao hilo ni la 10 kumbuka kwa Jeremiah Juma.Bao la Yanga limefungwa na Amisi Tambwe dakika ya 35. Bao la 14 kwa Amisi Tambwe msimu huu.