Thursday, February 25, 2016

WACHEZAJI TWIGA STARS WALIPOTEMBELEA DUKA LA AIRTEL


Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel , Juma Hassan akitoa maelezo ya jinsi ya kupata huduma mbalimbali za kisasa kwa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars walipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo liliko Morocco jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars wakimfatilia kwa makini Ofisa wa huduma kwa wateja wa Airtel Bw Stephen Makongoro wakati alipokuwa akitoa maelezo ya huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. Twiga Stars ilitembelea duka jipya la Airtel Expo lililopo jijini Dar es salaam.
Baadhi Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars wakitumia vifaa mbalimbali pamoja na simu za kisasa zilizopo katika duka la Airtel Expo wakati timu hiyo ilipotembelea duka hilio Jana, akishuhudia ni Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel , Boaz
Kikosi kizima cha timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars pamoja na uongozi wa timu hiyo na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati timu hiyo ilipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo lililopo Morocco jijini Dar Es Salaam.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Adriana Lyamba (nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars ambao wametokana na matunda ya mpango wa kuinua soka la vijana chini ya miaka 17 wa Airtel Rising Stars.