Monday, February 22, 2016

WACHEZAJI WA ARSENAL WAKIJIFUA KUJIWEKA SAWA DHIDI YA BARCELONA KWENYE UEFA CHAMPIONS LEAGUE! WENGER ASEMA WATAMLINDA SUAREZ.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema wachezaji wa Arsenal sharti wamnyamazishe Luis Suarez ndipo waweze kuwashinda Barcelona katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Arsenal watakuwa wenyeji wa Barca mechi ya mkondo wa kwanza katika hatua ya 16 bora Jumanne.
Barcelona, chini ya Luis Enrique, wamecheza mechi 32 ligini na katika kombe bila kushindwa, na Suarez amewafungia mabao 12 katika mechi saba alizocheza majuzi.
"Suarez ni mchezaji anayeweza kuunda moyo fulani kwenye timu,” amesema Wenger, aliyejaribu kumnunua Suarez Julai 2013 mchezaji huyo alipokuwa Liverpool.
 Arsene Wenger akiwaangalia Vijana wake

KESHO Jumanne Usiku Arsenal wana kimbembe kikubwa Uwanjani kwao Emirates watakapocheza Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, dhidi ya Mabingwa Watetezi FC Barcelona.
Lakini Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anategemea Kipa wake Petr Cech ataendeleza rekodi yake ya kutowahi kufungwa Goli na Lionel Messi.
Katika Mechi 8 akiwa Kipa wa Chelsea, Cech hajafungwa na Messi na Miaka Minne iliyopita alisaidia kuibwaga Barca kwenye Nusu Fainali ya UCL na pia kuwahi kuokoa Penati ya Messi wakati Chelsea waliposhinda na kutinga Fainali ambako walitwaa Kombe.
Wenger amejiliwaza kwa kusema: “Natumai Cech atatupa moyo mkubwa na atamtuliza Messi. Natumai Messi ataweweseka na historia kuwa upande wetu!”
Hata hivyo Barca ya sasa si Messi peke yake kwani Mashambulizi yao ni ya Mtu 3 wakiwepo pia Luis Suarez na Neymar.
Kipa Petr Cech

Washambuliaji wenzake Suarez, Lionel Messi, 28, na Neymar, pia huenda wakashirikiana safu ya mashambulizi dhidi ya Arsenal uwanjani Emirates.
Suarez, 29, ndiye anayeongoza kwa ufungaji mabao La Liga akiwa na mabao 25 na Wenger ameongeza: “Ni lazima tumnyamazishe Jumanne jioni.
“Ninaamini kando na ustadi wa kibinafsi wa washambuliaji hao watatu, huwa wanaelewana sana na kucheza vyema pamoja.
"Ninaamini Suarez husaidia sana timu. Alifanya hivyo akiwa Liverpool, na vile vile akicheza na Edinson Cavani na Diego Forlan [timu ya taifa ya Uruguay].

Walcott

Gnabry

Hii ni mara ya 3 kwa Arsenal kukutana na Barca kwenye hatua hii ya Mashindano haya na mara zote mbili za, Mwaka 2010 na 2011, walibwagwa nje ingawa 2011 walishinda Mechi ya Kwanza Bao 2-1 kwa Bao za Robin van Persie na Andrei Arshavin.
Arsenal, ambao Miaka 10 iliyopita walibwagwa 2-1 na Barca kwenye Fainali ya UCL ambayo Kipa wao Jens Lehmann alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu mapema kwenye Fainali hiyo, wanajipa sana moyo pale Meneja wao Wenger alipoeleza: “Barca ndio ‘Washindi Watarajiwa’ hivyo inabidi sisi tucheze Gemu ya juu kabisa. Lazima tuwe na mkazo. Tujiamini na tujitume!”
Danny Welbeck

 Alex Oxlade-Chamberlain

(L-R) Per Mertesacker, Aaron Ramsey, Theo Walcott na Calum Chambers

Olivier Giroud

(L-R) Kieran Gibbs, Welbeck, Mohamed Elneny, Oxlade-Chamberlain na Sanchez

Meneja Wenger

Mesut Ozil (kati)

Mikel Arteta na Gabrielkwa mbali

Sanchez kwenye zoezi leo jumatatu

 Petr Cech na David Ospina

Theo Walcott

Alex Iwobi

Arsenal, ambao walimaliza Nafasi ya Pili kwenye Kundi F nyuma ya Bayern Munich, ndio Timu pekee pamoja na Real Madrid kuingia Hatua za Mtoano za UCL kila Msimu tangu Mashindano haya yatumie Mfumo mpya kuanzia Msimu wa 2003/04.
Lakini katika Misimu Mitano iliyopita, Arsenal wamekuwa wakitupwa nje kwenye hatua hii.
Barcelona, waliomaliza Washindi wa Kundi E mbele ya AS Roma, wamekuwa wakitinga Hatua za Mtoano za UCL kwa Misimu 12 hadi sasa na wamefika Nusu Fainali mara 7 kati ya 8 zilizopita. Mara pekee ambayo walitolewa Robo Fainali katika kipindi hicho ni Msimu wa 2013/14 walipobwagwa na Atletico Madrid.
Katika Misimu 10 iliyopita, Barca wametwaa Ubingwa wa Ulaya mara 4.
Petr Cech