Thursday, February 18, 2016

WAYNE ROONEY NJE WIKI 6

KEPTENI wa Manchester United na England Wayne Rooney atakuwa nje kwa takriban Wiki 6 akiuguza Goti lake.
Inasemekana Rooney aliumia Wikiendi iliyopita Man United walipofungwa na Sunderland na sasa yupo hatarini kuzikosa Mechi 8 za Timu yake zikiwemo zile dhidi ya Arsenal, Man City na Tottenham.
Jana Meneja wa Man United Louis van Gaal aliongea huko Denmark ambako Leo wanacheza Mechi ya Europa Ligi na FC Midtjylland na kugusia kuhusu kuumia kwa Rooney lakini hakutaja atakuwa nje muda gani.
Van Gaal alisema: "Anatufungia Bao nyingi na hivyo ni muhimu kwetu. Inabidi twende bila yeye."
Rooney, mwenye Miaka 30, hayupo huko Denmark na licha ya kuumia kwenye Mechi na Sunderland aliimaliza Mechi yote hiyo na Van Gaal amezungumzia hilo.
"Ni Mtu anaetaka kuendelea hadi mwisho hata kama kaumia. Anataka kushinda tu! Ni hulka nzuri lakini wakati mwingine inaumiza mwili wake!"
Man United wapo Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 6 nyuma ya Timu ya 4 Man City na kumkosa Kepteni wao ni pigo kwao katika azma yao ya kumaliza ndani ya 4 Bora.
Pia, Timu ya Taifa ya England ambayo Mwezi Juni itacheza Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, huki France, itamkosa kwenye Mechi zao 2 za Kirafiki Mwezi Machi dhidi ya Germany na Netherlands.