Sunday, February 7, 2016

YANGA YAUA 4-0 TAIFA LEO! MAAFANDE JKT RUVU HOI!!

Mabingwa Watetezi Yanga wameendelea kuongoza Ligi Kuu Vodacom, VPL, baada ya kuichapa JKT Ruvu 4-0 kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Huko Shinyanga, Simba iliitungua Kagera Sugar kwa Bao la Ibrahim Ajib wakati Chamazi Complex, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC iliitungua Mwadui FC bao 1-0 kwa goli la Kipre Tchetche.
Bao za Yanga hii Leo zilifungwa mbili na Simon Msuva na nyingine kupitia Issofou Boubacar na Donald Ngoma.

Ushindi huu umewabakiza Yanga kileleni wakiwa na Pointi 43 kwa Mechi 18 wakifuatiwa na Simba wenye na Pointi 42 kwa Mechi 18 huku Azam FC ikiwa na Pointi 42 kwa Mechi 16.

Kwa Yanga hii ni faraja kubwa baada ya kuchapwa 2-0 na Coastal Union huko Tanga na kisha kutoka 2-2 na Tanzania Prisons katika Mechi zao 2 zilizopita.