Monday, March 14, 2016

AFRICAN SPORTS YAICHAPA MBEYA CITY BAO 2-0 VPL!

BAO 2 za Issa, Leo zimewapa African Sports ushindi wa 2-0 walipocheza na Mbeya City huko Mkwakwani, Tanga katika Mechi pekee ya VPL, Ligi Kuu Vodacom.
Bao zote hizo zilifungwa Kipindi cha Pili na kuifanya Sports ijikwamue kutoka mkiani na kuwashusha Mahasimu wao wakubwa wa Jijini Tanga Coastal Union washike mkia.
Baada ya Mechi 23 kwa kila Timu, African Sports wapo Nafasi ya 15 wakiwa na Pointi 20 na Coastal wapo Nafasi ya 16 ambayo ni ya mwisho wakiwa na Pointi 19.
Mbeya City wamebaki palepale Nafasi ya 9.
VPL inaongozwa na Simba waliocheza Mechi 23 na wana Pointi 54, wakifuata Yanga wenye Pointi 50 kwa Mechi 21 na ya 3 ni Azam FC yenye Pointi 47 kwa Mechi 20.