Tuesday, March 15, 2016

ATAWEZA? RAFA BENITEZ AANZA NA KICHAPO NEWCASTLE UNITED!


Rafa Benitez
Leicester City wamepanua uongozi wao kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupata ushindi dhidi ya Newcastle.
Lecester walilaza Newcastle, waliokuwa wakicheza mechi yao ya kwanza chini ya meneja mpya Rafael Benitez, kwa bao 1-0 mechi hiyo iliyochezwa Jumatatu usiku.
Shinji Okazaki ndiye aliyewafungia bao hilo la pekee, na alilifunga kwa ustadi wa aina yake dakika ya 25. Image caption Shinji akifunga bao
Leicester City sasa wanazidi kukaribia kushinda taji lao la kwanza kabisa la ligi zikiwa zimesalia mechi nane msimu huu.
Newcastle walionekana kuimarika na walikaribia kufunga kupitia Ayoze Perez na Moussa Sissoko lakini bahati yao haikusimama.


Kabla ya mechi hiyo, meneja wa Leciester Claudio Ranieri alikataa kukubali kwamba ndio wanaopigiwa upatu kushinda ligi.
Badala yake, alisisitiza kuwa lengo lao ni kufuzu kwa Europa League.
Vijana hao wa Ranieri kwa sasa wamo alama 12 mbele ya Manchester City na 11 mbele ya Arsenal, jambo linalowafanya wengi kuamini kwamba sasa vita vya kushindania ligi ni kati yao na Tottenham walio nambari mbili.
Kwa Newcastle, mechi mbili zijazo zitakuwa muhimu katika kufufua matumaini yao ya kutaka kusalia ligi kuu.
Watakuwa wenyeji wa Sunderland Jumapili kisha wakutane na Norwich ugenini tarehe 2 Aprili.
Leicester watasafiri kukutana na Crystal Palace Jumamosi.


Mechi zijazo za Leicester City:

Jumamosi 19 Machi 2016
Crystal Palace vs Leicester 18:00

Jumapili 3 Aprili 2016
Leicester vs Southampton 16:30

Jumapili 10 Aprili 2016
Sunderland vs Leicester 16:30

Jumapili 17 Aprili 2016
Leicester vs West Ham 16:30