Wednesday, March 16, 2016

BARCELONA vs ARSENAL LEO HII JUMATANO KIONGOZI BARCA ASEMA ‘WATAJITUMA MPAKA MWISHO!!

KOCHA wa Barcelona Luis Enrique amesema wao hawabweteki na hawatilii maanani kuwa na faida baada ya kuifunga Arsenal 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI huko Emirates bali wataingia ngangari katika Mechi ya Marudiano Jumatano Usiku huko Nou Camp.
Barca wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawajafungwa katika Mechi 37 na wameshinda Mechi zao 8 zilizopita huku wakiwania kutinga Robo Fainali ya UCL kwa mara ya 10 mfululizo.
Katika Mechi ya kwanza huko Emirates, Bao 2 za Mchezaji Bora Duniani, Lionel Messi, ndizo ziliwapa Barca ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal.

Mshindi wa Mechi hii atatinga Robo Fainali ya UCL.
Mechi zao zilizopita za Wikiendi:
Barcelona 6-0 Getafe (Juan Rodríguez 8 Kajifunga, El Haddadi 19, Neymar 32 51, Messi 40, Arda Turan 57)
-Ushindi huu umezidi kuwachimbia Barca kileleni mwa La Liga.
Arsenal 1-2 Watford (Ighalo 50, Guedioura 63; Welbeck 88)
-Kipigo hiki kiliwatupa Arsenal nje ya FA CUP ambayo wao walikuwa Mabingwa Watetezi kwa Misimu Miwili iliyopita.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Barcelona:
Ter Stegen; Alves, Mathieu, Mascherano, Alba; Busquets; Rakitić, Iniesta; Messi, Suárez, Neymar.

Hawatacheza: Rafinha (Goti), Sandro (Musuli), Piqué (Kifungo)
Arsenal: Ospina; Bellerín, Mertesacker, Gabriel, Monreal; Coquelin, Elneny; Campbell, Özil, Sánchez; Giroud.
Hawatacheza: Ramsey (Paja), Čech (Musuli), Cazorla (Kifundo cha Mguu), Oxlade-Chamberlain (Goti), Rosický (Paja), Wilshere (Mguu)

Hatihati: Koscielny (Tatizo la Mguu)
REFA: Sergei Karasev (Russia)
UEFA CHAMPIONS LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
Saa 4 Dakika 45 Usiku

Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza

JUMANNE 15 MAR 2016

Atletico Madrid vs PSV Eindhoven [0-0]
Man City vs Dynamo Kiev [3-1]

JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona vs Arsenal [2-0]
Bayern Munich v Juventus [2-2]