Sunday, March 13, 2016

FULL TIME...FA CUP: ARSENAL 1 vs 2 WATFORD, IGHALO NA GUEDIOURA WAICHAPA GUNNERS! ARSENAL WATUPWA NJE!


ARSENAL, wakiwa kwao Emirates, Leo wamepoteza Taji lao la Miaka Miwili mfululizo baada ya kufungwa 2-1 na Watford kwenye Robo Fainali ya EMIRATES FA CUP.
Bao zilizoiua Arsenali zilifungwa na Odion Ighalo na Adlene Guedioura katika Dakika za 50 na 63 na Arsenal kupata kifutia machozi toka kwa Danny Welbeck Dakika ya 88 ambae pia alikosa Bao la wazi la kusawazisha Dakika za Majeruhi.
Watford sasa wanaungana na Crystal Palace na Everton kwenye Robo Fainali na Timu ya 4 itapatikana baada ya kupatikana Mshindi kati ya Man United na West Ham.

Bao za Watford zimeanza kufungwa kipindi cha pili dakika ya 50 kupitia kwa Odion Ighalo  na bao la pili limefungwa na Adléne Guédioura dakika 63 kwa shuti kali lililomzidi ujanja kipa wa Arsenal David Ospina. 
Bao la Arsenal limefungwa na Danny Welbeck dakika ya 88 baada ya kufanya shambulizi kali.
1-0

GabrielAlexis SanchezArsene WengerTheo WalcottKipa David Ospina