Thursday, March 3, 2016

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: BELGIUM NI KISIKI NI YA 1, TANZANIA IPO PALE PALE 125! SPAIN YA 3, ARGENTINA YA PILI!

Belgium wameendelea kuwa ndio Timu Bora Duniani wakifuatiwa na Argentina na Spain kwa mujibu wa Listi ya Ubora iliyotolewa Leo na FIFA.
Mabingwa wa Dunia Germany wapo Nafasi ya 4 na katika 20 Bora Nchi pekee iliyobadilisha Nafasi ni Italy ambayo imepanda Nafasi 1 kushika Nafasi ya 14 ikiwa juu ya Netherlands ambayo ni ya 15.
Kwa Afrika, Timu Bora ni Cpe Verde ambayo iko Nafasi ya 31 ikifuatiwa na Ivory Coast inayoshika Nafasi ya 36 na Algeria ya 37.
Tanzania imebakia Nafasi yake ile ile ya 125.

Listi ya Ubora nyingine itatolewa Tarehe 7 Aprili.
10 BORA HII:
1. Belgium
2. Argentina
3. Spain
4. Germany
5. Chile
6. Brazil
7. Portugal
8. Colombia
9. England
10. Austria